قال الشيخ العلامة صالح الفوزان – حفظه الله تعالى
Amesema Sheikh mwanachuoni Swaaleh Al-Fawzaan – Allaah amuhifadhi:
والانحراف عن العقيدة الصحيحة له أسباب تَجِبُ معرفتها، من أهمها
“Kupotoka kutoka kwenye itikadi sahihi kuna sababu ni wajibu kuzitambua, muhimu katika hizo:
١ – الجهلُ بالعقيدة الصحيحة
1 – Ujinga kutokuijua itikadi sahihi.
٢ – التّعصُّبُ لما عليه الآباء والأجداد، والتمسك به وإن كان باطلاً، وتركُ ما خالفه وإن كان حقًّا
2 – Kuwa na Taa’sub / Kunusuru mambo waliyonayo mababa na mababu, na kushikamana nayo hata yakiwa batili, na kuacha yaliyo kinyume na hayo hata yakiwa ni haki.
٣ – التقليدُ الأعمى بأخذِ أقوال الناس في العقيدة من غير معرفة دليلها، ومعرفة مدى صحتها
3 – Kuiga kwa upofu kwa kuchukua kauli za watu kwenye itikadi bila kujua dalili zake, na kujua usahihi wake.
٤ – الغُلُو في الأولياء والصالحين، ورفعهم فوق منزلتهم؛ بحيث يُعتقد فيهم ما لا يَقدِر عليه إلا الله
4 – Kuvuka mipaka kwa vipenzi / wema wa Allaah, na kuwanyanyua juu zaidi ya daraja lao, kwa kiasi kwamba wanaitikadiwa mambo wasiyoyaweza isipokuwa Allaah.
٥ – الغفلة عن تَدَبُّر آيات الله الكونية، وآيات الله القرآنية، والانبهار بمعطيات الحضارة المادية؛ حتى ظنوا أنها من مقدور البشر وحده؛ فصاروا يُعظِّمون البشر
5 – Kughafilika na kuacha kuzingatia aya za Allah za uumbaji, na aya za Allah za Qur’aan, na kufurahishwa na vitu watu walivyopewa katika tamaduni za maendeleo, mpaka wakadhani kwamba ni uwezo wa binadamu pekee, wakawa wanawatukuza binadamu.
٦ – أصبح البيتُ في الغالب خاليًا من التوجيه السليم
6 – Nyumba zimekuwa mara nyingi zimeepukana na miongozo iliyokuwa salama.
“.٧ – إحجامُ وسائل التعليم والإعلام في غالب العالم الإسلامي عن أداء مهمتها
7 – Vyombo vya elimu na vyombo vya habari sehemu nyingi ya ulimwengu kuacha kutekeleza majukumu yake.”
📚 عقيدة التوحيد (١٣/١١)
_________________
Mfasiri: Sheikh Abuu Khaythamah Swaabun
Imechapishwa na: https://www.manhajmedia.com
Marejeo: |[ Kitabu: ‘Aqiydat At Tawheed (11/13) ]|
⛔️ Usibadili chochote, sambaza kama ulivyoipokea.