قال الشيخ ربيع بن هادي – حفظه الله
« فالإخوان المسلمون أخطر الفِرق على الإسلام منذ قامت دعوة الإخوان المسلمين، وهم من أكذب الفرق بعد الروافض »
Amesema Sheikh Rabii bin Haadiy ( Allâh amuhifadhi ):
“Ikhwaan-ul-Muslimun ni kundi hatari zaidi kwa Uislamu tangia ulipoanza ulinganizi wao, nao ndio kundi ambalo ni waongo zaidi baada ya Mashia.”
Maelezo:
Kauli hii ya Shaykh Rabi’i bin Haadi al-Madkhali ni ukosoaji mkali dhidi ya kundi la al-Ikhwan al-Muslimun, kundi maarufu la kisiasa na kidini lililoanzishwa nchini Misri mwaka 1928 na Hasan al-Bannaa.
⚠️ Miongoni mwa makosa yao:-
1. Kutumia dini kufikia malengo ya kisiasa.
2. Kupuuzia misingi ya itikadi (Aqiydah) ya Salaf (wema waliotangulia).
3. Kushirikiana na makundi ya bid‘ah na hata wasiokuwa Waislamu kwa sababu za kisiasa.
_________________
Mfasiri: Ustadhi Abuu Mujtaba Ahmad Mwinyiwiwa
Imechapishwa na: https://www.manhajmedia.com
Marejeo: |[ المصدر : تاريخ (28-9-1437 ) ]|
Tarehe: 24-Shawwal-1446H | Jumanne 22-April-2025M
Sehemu: Kibaha – Pwani – Tanzania.
⛔️ Usibadili chochote, sambaza kama ulivyoipokea.