Sheikh Muhammad Mujahid (Abuu Abdis-Salam) حفظه الله

Sheikh Muhammad Mujahid (Abuu Abdis-Salam) حفظه الله

Sheikh Abuu Abdis Salam Muhammad Mujahid حفظه الله ni miongoni mwa Masheikh (walezi) na walinganizi wa Dini ya Kiislam nchini Tanzania, mwenye juhudi kubwa katika kufundisha na kusambaza elimu ya Uislamu kwa kufuata Manhaj ya Salafus-Saalih. Amejikita katika kufundisha masomo mbalimbali ya kisheria kupitia Qur’aan tukufu na Sunnah za Mtume ﷺ.

Amechangia kwa kiasi kikubwa katika kuelimisha jamii kupitia Mihadhara, Darsa, Semina na Khutba mbalimbali za Ijumaa, ambapo hulenga kujenga uelewa sahihi wa Aqeedah (Itikadi), Fiqh na mwenendo sahihi wa Muislamu katika maisha ya kila siku.

Sheikh anaendelea kushiriki katika utoaji wa elimu kupitia Markaz na Masjid Omar bin Khattab iliyopo Kariakoo mtaa wa Jangwani (akiwa kama Mudiru wa Markaz hiyo), ikiwemo vipindi vya moja kwa moja (live) na sauti zilizorekodi zinazowafikia Waislamu ndani na nje ya nchi.

Title
.