Sheikh Dr. Khamiis Imaam حفظه الله

Sheikh Dr. Khamiis Imaam حفظه الله

Sheikh Dr. Khamiis Imaam حفظه الله ni miongoni mwa Masheikh na Walinganizi wa Kiislamu wanaojishughulisha na kufundisha na kueneza elimu ya dini kwa kufuata Qur-aan na Sunnah kwa uelewa wa Salafus-Swaalih. Ana elimu ya juu katika masomo ya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na shahada ya uzamivu (PhD), na amepata elimu yake kutoka kwa wanazuoni mbalimbali wanaofuata manhaj ya Salaf. Ni miongoni mwa masheikh wa Masjid Omar bin Khattwab, na pia ni msimamizi wa Diploma ya Sheria katika Markaz Omar bin Khattwab – Kariakoo, Dar es Salaam. Amejikita katika kufundisha masomo ya Dini kama vile ‘Aqiydah (itikadi), Fiqh (sheria za Kiislamu) nakadhaalika.

Katika da‘wah yake, Sheikh Dr. Khamiis Imaam anajulikana kwa kusisitiza na kuhimiza watu kushikamana na Manhaj ya Salafus-Swaalih, Tawheed, pamoja na kupinga bid‘ah na mambo yasiyokuwa na msingi sahihi katika dini. Amechangia kwa kiasi kikubwa katika kueneza elimu kupitia Darsa, Mihadhara, Semina na Khutba za Ijumaa. Njia yake ya ufundishaji ni ya wazi, yenye hoja na inayolenga kuwafikisha watu kwenye uelewa sahihi wa dini.

Title
.