Sheikh Abuu Muhammad Jaafar Swaleh Al-Humeidy حفظه الله

Sheikh Abuu Muhammad Jaafar Swaleh Al-Humeidy حفظه الله

Sheikh Abuu Muhammad Jaafar Swaleh Al-Humeidy حفظه الله Ni katika Masheikh wakubwa wa Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah nchini Tanzania, na ni miongoni mwa walinganiaji mashuhuri wa Da’wah Salafiyyah katika Mkoa wa Kigoma na maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Sheikh Jaafar Swaleh Al-Humeidy anafahamika kwa juhudi zake kubwa katika kueneza Aqiydah Sahihi ya Tawhiyd, kufundisha Sunnah za Mtume ﷺ, na kuwalingania Waislamu kushikamana na Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu wa Salafus-Swaalih.

Ni katika Masheikh wanaoaminika kwa elimu yao, msimamo wao wa Manhaj, na hikmah yao katika kulingania Dini ya Allaah. Amebahatika kusoma na kuchukua elimu kutoka kwa Wanachuoni wakubwa nchini Saudi Arabia, jambo lililompa msingi imara katika elimu za Aqiydah, Fiqh, Hadiyth na Manhaj.

Katika shughuli zake za Da’wah, Sheikh Jaafar amekuwa mstari wa mbele katika:

  • Kulingania Tawhiyd na kumpwekesha Allaah katika ibada zote.
  • Kueneza na Kuhuisha Sunnah na kutoa mafundisho sahihi ya Uislamu.
  • Kupinga Bid’ah, Khuraafaat na itikadi potofu zinazokinzana na Qur-aan na Sunnah.
  • Kuwalea wanafunzi wa elimu ya Dini na kuwahimiza Waislamu kushikamana na njia ya Maswahaba na Salafus-Swaalih.
  • Kukuza umoja wa Waislamu juu ya haki kwa mujibu wa dalili sahihi za Kiislamu.

Tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى amzidishie elimu yenye manufaa, ikhlasi, afya njema na aibariki juhudi zake katika kuieneza Dini ya Uislamu na kuwatumikia Waislamu.

Title
.