:السؤال
ما حكم استعمال أدوات التجميل للنساء وما حكم بيعها؟
:الجواب
قال الشيخ الألباني رحمه الله: أرى أن بيع أدوات التجميل المعروفة اليوم لا يجوز! لأن ذلك من عادة الكافرات أو الفاسقات من المسلمات بناءً على هذا وعلى النصوص التي تَعْرفها من النهي عن التشبُّهِ بالكفَّار. وما فيه إضافة إلى ذلك من تغيير خلق الله عز وجل فلا أرى جواز الاستعمال؛ بالتالي لا أرى جواز البيع أو الشراء
السائل: طيب إن كان هذا مما يطلبه الزوج ويبعث على المودة والألفة بين الزوجين؟
الألباني رحمه الله: له أن يطلب منها ما يجيزه الشرع؛ وما لا يجيزه الشرع فلا، له منها أن يطلب ما يجيزه الشرع
السائل: فإن كانت مغلوبة على أمرها يعني إن لم تفعل صار انشقاق ونحو ذلك هل لها مع علمها أنه مُحرَّم أن تفعله خشية أن تدمر حياتها؟
الألباني رحمه الله: لا طاعة لمخلوق في معصية الخالق
Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia vipodozi kwa wanawake, na ipi hukumu ya kuviuza?
Jibu: Sheikh Al-Albaani (Allah amrehemu) amesema:
“Ninaona kuwa kuuza vipodozi vinavyojulikana siku hizi hakufai (si halali). Kwa sababu hayo ni katika desturi za wanawake makafiri au wanawake waovu miongoni mwa Waislamu. Hii ni kwa kuzingatia jambo hilo pamoja na dalili mnazozijua zinazokataza kujifananisha na makafiri.
Na zaidi ya hayo, ndani yake kuna kubadili uumbaji wa Allah Aliyetukuka. Hivyo sioni kuwa inafaa kuvitumia, na kwa hiyo pia sioni kuwa inafaa kuviuza wala kuvinunua.”
Muulizaji anaendelea kuuliza: Vipi ikiwa jambo hilo ni katika yale anayoyataka mume, na yanaleta mapenzi na maelewano kati ya wanandoa?
Sheikh (Allah amrehemu) anaendelea kujibu:
“Anaruhusiwa kumtaka mke wake yale ambayo Sheria imeyaruhusu. Ama yale ambayo Sheria haikuyaruhusu, basi haruhusiwi kuyataka. Ana haki ya kumtaka yale ambayo Sheria imehalalisha.”
Muulizaji: Ikiwa mwanamke yuko katika hali ya kushinikizwa, yaani asipofanya hivyo kutatokea migogoro au mfano wa hayo, je, inamruhusu kufanya jambo hilo huku akijua kuwa ni haramu, kwa kuhofia maisha yake ya ndoa kuharibika?
Sheikh Al-Albani (Allah amrehemu): “Hakuna kumtii kiumbe katika kumuasi Muumba.”
_________________
Mfasiri: Sheikh Abuu Mujtaba Mwinyiwiwa
Imechapishwa na: https://www.manhajmedia.com
Marejeo: |[ سلسلة الهدى والنور : شريط (42) ]|
⛔️ Usibadili chochote, sambaza kama ulivyoipokea.