سلامتك في التمسك بمنهج سلف الصالح

SALAMA YAKO EWE MUISILAMU IPO KATIKA KUFUATA NJIA YA WEMA WALIOTANGULIA:

قال الشيخ صالح الفوزان حفظه الله: ( إذا أردت النجاة وأردت السعادة وأردت السلامة من الضلال فعليك بمنهج السلف)

شرح الدرة المضية في عقد أهل الفرقة المرضية، ( ص: ٢٧٨ )

Amesema Sheikh Swaaleh Al-Fawzaan – Allaah amuhifadhi:

“Ukitaka kuokoka na ukataka Utukufu na ukataka kusalimika kutokana na upotevu basi ni juu yako Ushikamane na Manhaj Salaf-us-Swaaleh (Njia ya Wema waliotangulia).”

Maelezo ya mfasiri:- Allaah amuhifadhi

Ndugu msomaji wa maneno haya ya Sheikh – Allah amuhifadhi, yako wazi kabisa na yanatuzindua kwa kiasi kikubwa sana kwamba: Mwenye kutaka kuokoka na adhabu za Allah na mwenye kutaka Utukufu hapa Duniani na kesho Siku ya Malipo na mwenye kutaka salama ili asalimike na upotevu na maangamivu, basi ni juu yake mtu huyo ashikamane na njia moja tu, njia ya wema walio tangulia na si vinginevyo.

Na kinyume chake ni kwamba asiyetaka kuokoka na kusalimika kutokana na upotevu na asiyetaka utukufu, basi aache kufuata njia ya Wema Waliotangulia (Manhaj Salaf-us-Swaaleh).

Tunajifuza katika maneno haya ya Sheikh (Allah amuhifadhi) kwamba: Kheri zote zipo katika kufuata Manhaj Salaf-us- Swaaleh na shari zote zipo katika kukhaalifu njia hiyo ambayo ndio njia ya Mtume Muhammad – SwallaAllahu ‘alayhi wasallam.

Twamuomba Allah mtukufu aturuzuku Taq-wa na Ikhlaasw katika matendo yetu na atuthibitishe katika Manhaj Salaf hadi mwisho wa uhai wetu.

_________________

Mfasiri: Sheikh Abuu AbdilWahhab Ilyasaa Juma
Imechapishwa na: https://www.manhajmedia.com
Marejeo: |[ Tazama kitabu: Sharhu Ad-Durratil-Mudhweiyya Fi Aqadi Ahlil-firqatil-Mardhwiyya – Ukurasa wa (278)
]|

⛔️ Usibadili chochote, sambaza kama ulivyoipokea.