Huna chako katika Mali yako ispokuwa Mali tatu tu.

:ليس لك من مالك إلا ثلاث

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ” يقول العبد : مالي مالي، إنما له من ماله ثلاث : ما أكل فأفنى، أو لبس فأبلى، أو أعطى فاقتنى، وما سوى ذلك فهو ذاهب وتاركه للناس

رواه مسلم : 2959

Hadithi:
Kutoka kwa Abii Hurayra – Allah amridhie – kwamba Mtume – Swalla Allahu ‘alayhi wasallam amesema:

Anasema mja: Mali yangu ni mali yangu, hakika si vinginevyo chake yeye katika mali yake ni mali tatu tu:

1) Mali ya kwanza ni kile chakula alichokula kikaisha.
2) Au nguo aliyoivaa hadi akaimaliza.
3) Au mali aliyoitoa akatarajia thawabu zake kwa Allah, na mali nyengine zote zisizokuwa hizo basi yeye (mwanadamu) ataondoka (duniani) atawaachia watu.”

Maelezo ya mfasiri – Allah amuhifadhi:

Ndugu msomaji wa makala hii katika hadithi hii ya Mtume – Swalla Allahu ‘alayhi wasallam tunajifuza mambo mengi sana lakini mingoni mwayo ni haya yafuatayo:

1) Kwamba Mtume – Swalla Allahu ‘alayhi wasallam anaubainishia Umma wake kuwa mwanadamu hana chake katika mali yake zaidi ya chakula alichokula kikaisha, au nguo aliyoivaa hadi ikaisha, au mali aliyoitoa ikakubaliwa.

2) Na kwamba mali ambayo mwanadamu hajaitumia ikaisha hiyo si yake bali ni ya warithi wake yeye muda wowote ni mwenye kuondoka duniani mali hiyo ataiacha watu watabaki wanaigombania.

3) Pia katika hadithi hii tunajifunza umuhimu wa kutoa Mali katika njia zake zote za kheri na hiyo ndio Mali yenye kumsaidia mja baada ya kufa kwake.

Kwa hiyo ndugu msomaji usiendekeze kuchuma Mali na kuihesabu tu ilihali hata kula hauli vizuri wala huvai vizuri wala huitoi Mali hiyo katika njia za kheri, fahamu kwamba siku yoyote utakufa na mali hiyo utaiacha.

Allah atujalie mwisho mwema.

_________________

Mfasiri: Sheikh Abuu AbdilWahhab Ilyasaa Juma
Imechapishwa na: https://www.manhajmedia.com
Marejeo: |[ Hadithi ameipokea imamu Muslim: 2959 ]|

⛔️ Usibadili chochote, sambaza kama ulivyoipokea.